SUMATRA yawaruka wamiliki wa pikipiki
Na Dunstan Bahai

MAMLAKA ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), imesema haijawahi kutoa leseni kwa pikipiki za matairi mawili na matatu (Bajaj) na kwamba kuwapo kwa biashara hiyo ni kinyume na sheria.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Meneja wa Mawasiliano kwa Umma wa mamlaka hayo David Mziray, wakati akizungumza na gazeti hili.

Alisema mbali na leseni, biashara hiyo haina bima ya biashara, kwani bima iliyopo ni ya chombo na kwamba mamlaka imekuwa ikiwasisitiza wamiliki na waendeshaji kukata bima hiyo kwa ajili ya usalama wa abiria.

Mziray alisema, ili kuhalalisha biashara hiyo iendeshwe kiusalama zaidi, SUMATRA ipo kwenye mchakato wa kukusanya maoni ya wadau mbalimbali, ili zitungwe kanuni na sheria za kusimamia biashara hiyo.

“Tupo kwenye kukusanya maoni kutoka kwa wadau mbalimbali, ili tuweze kutunga kanuni za kusimamia biashara hiyo na baadaye tunazipeleka wizarani na kisha kwa Mwanasheria Mkuu, akizipitisha tu biashara hiyo itaanza,” alisema.

Mapema mwaka huu, Serikali kupitia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ilikubali kutambua usafiri wa pikipiki na Bajaj kutoa huduma ya kusafirisha abiria kwa malipo au kukodisha. Akifungua mkutano wa kukusanya maoni ya wadau mwezi uliopita, Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA Israel Sekirasa, alisema aina hiyo ya usafiri si salama sana.

“Ukweli ni kwamba vyombo hivi si salama sana, na vinaendana na matukio ya ajali, wizi, unyang'anyi zaidi kuliko usafiri mwingine,” alisema Sekirasa.

Alisema Serikali ilitoa uamuzi wa kutumika kwa usafiri huo kwa tahadhari kubwa kwa kuzingatia kuwa maeneo mengi ya mijini na yale ya vijijini hayafikiki kwa magari, na kwa kutambua kuwa ni sehemu ya ajira kwa vijana.

Wiki iliyopita, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam iliamua kusimamishwa kwa muda huduma ya vyombo hivyo kubeba abiria, wakati serikali ikiwaandalia utaratibu wa kiusalama zaidi.

Hata hivyo, waendesha pikipiki na Bajaj walipinga vikali hatua hiyo, na kuiomba Serikali wakati ikiandaa utaratibu iwaruhusu kuendelea na biashara yao.

Maoni

Jina

Barua Pepe

 


Logo Logo
||Mtanzania|| Bingwa|| Rai|| Dimba|| The African||
TANGAZA NASI
Click to View National Business Directory Details
Home
Maoni ya Mhariri
Habari za Kitaifa
Habari za Kimataifa
Wazo Binafsi
Makala na Barua
Udhamini
Biashara
Elimu na Jamii
Michezo
Burudani
Directory 2010
Wasiliana Nasi