TULIKUWA TUNAITAKA SIMBA MWAKA HUU
Na Kambi Mbwana
UONGOZI wa klabu ya Yanga, umesema walikuwa wana hamu ya kukutana na Simba kabla mwaka huu haujamalizika ili waweze kulipiza kisasi cha kufungwa bao 1-0 katika mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya soka Tanzania bara.
Akizungumza jana, Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako alisema kuwa wamefurahi sana kukutana na Simba katika mchezo wa nusu fainali.
“Tulikuwa tuna hamu kubwa ya kukutana na Simba lakini Mungu ametujalia kukutana na mnyama sasa nawaeleza mashabiki wote wa SImba wafahamu kuwa keshokutwa ni zamu yetu ya kushinda mchezo huo,” alisema Mwalusako
“Tumepania kweli kweli kuifunga Simba katika mchezo huo, hivi sasa tuna kocha mzuri mwenye uwezo wa juu, Kostadin Papic,” alisema.
.
Maoni
Jina
Barua Pepe