SHIMUTA KUKUTANA NA BMT, WAZIRI WA HABARI
Na Winfrida Ngonyani

UONGOZI mpya wa Shirikisho la Michezo ya Mashirika ya Umma na Makampuni Binafsi Tanzania, SHIMUTA, liko mbioni kukutana na Baraza la Michezo la Taifa BMT na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, George Mkuchika, kama njia mojawapo ya kujitambulisha.
Akuzungumza na Mtanzania jana, Katibu Mkuu wa SHIMUTA, Award Safari alisema, baada ya kujitambulisha BMT, pia watakutana na Mlezi wa shirikisho hilo, Makamu wa Rais, Ali Mohamed Shein.
“Lengo ni kutaka kuutambulisha uongozi mpya uliongia madarakani baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika mjini Tanga, ikiwa sambamba na kuelezea hali halisi ya shirikisho hilo ikiwa ni pamoja na kuiomba serikali kutoa tamko juu ya taasisi kushiriki michezo,” alisema.
Award alisema baadhi ya taasisi zimekuwa hazishiriki katika michezo hiyo baada ya kupitishwa kwa sera ya serikali ya ubinafsishaji wa mashirika ya umma, ambako amewataka kuacha kuchulia suala hilo kama kigezo cha kutoshiriki.
 “Tangu baadhi ya mashirika yabinafsishwe kumekuwa na muitikio mdogo wa kushiriki, sasa tulikuwa tumepanga tukutane na serikali ili, walisisitizie jambo hilo kwani michezo katika kazi ni njia mojawapo ya ufanisi,” alisema

katibu huyo kuwa, kikao cha shirikisho hilo kilichokaa Jumamosi iliyopita jijini Dar es Salaam kimeazimia kuwa, uchaguzi mkuu wa Halmashauri Kuu ufanyike mapema mwezi Machi, mwakani mjini Dodoma na wajumbe wamependekeza mashindano ya SHIMUTA mwakani yafanyike Arusha


Maoni

Jina

Barua Pepe

 


Logo Logo
||Mtanzania|| Bingwa|| Rai|| Dimba|| The African||
TANGAZA NASI
Click to View National Business Directory Details
Home
Maoni ya Mhariri
Habari za Kitaifa
Habari za Kimataifa
Wazo Binafsi
Makala na Barua
Udhamini
Biashara
Elimu na Jamii
Michezo
Burudani
Directory 2010
Wasiliana Nasi